Nyota wa timu ya taifa ya Argnetina Lionel Messi amesema ingekuwa “Ujinga” endapo taifa lake lisingefuzu kucheza fainali za kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

Messi ameyasema hayo alfajiri ya leo baada ya kuisadia timu yake kufuzu fainali hizo kwa kufunga Hat-trick kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Ecuador. Argentina ilikuwa inahitaji ushindi pekee katika mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu na imefanikiwa baada ya kushinda 3-1.

“Ingekuwa ni “Ujinga” kama tusingefuzu fainali tukiwa na kundi kubwa la wachezaji wazuri, hakika huwezi kufurahia kuwa nje ya fainali kwa timu kama Argentina” Messi amewaambia Wanahabari.

Argentina imeungana na mataifa ya Brazil, Uruguay na Colombia kutoka bara la Amerika Kusini maarufu CONMEBOL kwenda Urusi mwakani huku wakiiacha Peru ikisubiri kucheza mtoano dhidi ya New Zealand ili kufikisha idadi ya timu tano kutoka bara hilo kama itashinda.

Argentina imekuwa haina mwendelezo mzuri wa ushindi ama kushnda vikombe pamoja na kuwa na nyota wengi wenye vipaji vikubwa kama Kun Aguero, Paul Dybala, Angel Di Maria na Messi.

Ujumbe huo wa Messi umetafsiriwa kama dhihaka kwa wachezaji wenzake ambao wamekuwa hawampi msaada akicheza nao licha ya kuwa bora kwenye klabu zao.