Image result for simon msuva

Image result for telela





Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
WINGA wa kimataifa wa Tanzania, 
Simon Happugod Msuva amesema
 kwamba kiungo Salum Abdul Telela 
ni kati ya wachezaji waungwana 
aliokutana nao Yanga SC na hawezi 
kuwasahau kwa wema wao daima.
Msuva alikwenda kumtembelea 
Telela mwishoni mwa wiki kabla 
ya kurejea Morocco kufuatia kuja 
nchini kuichezea timu ya taifa mechi
 ya kirafiki dhidi ya Malawi Jumamosi.
Na mfungaji huyo wa bao la kusawazisha 
la Tanzania katika sare ya 1-1 Uwanja 
wa Uhuru mjini Dar es Salaam
 akaenda kumtembelea mchezaji
 mwenzake wa zamani wa Yanga
 baada ya mchezo huo.


“Nilikwenda kumtembelea Telala, 
kwa sababu ni rafiki yangu sana 
na tumetoka mbali, tuna historia, 
alinipokea vizuri Yanga na akaishi
 na mimi vizuri sana. Hata alipoondoka
 niliumia sana,”alisema Msuva akizungumza
 na Bin Zubeiry Sports – Online 
jana kwa simu kutoka Morocco.
Msuva amesema kwamba Telela

 ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa 
sana na ambaye anaweza kucheza timu
 yoyote nchi yoyote. “Mwenyewe
 ameamua kurudi masomoni,  mambo
 ya soka hayapi kipaumbele tena,
”amesema ambaye pia alitembelea 
timu yake ya zamani, Yanga mazoezini.