Mtuhumiwa Hatari wa Uporji na Mauaji Auwawa kwa Kupigwa Risasi na Polisi


Mkazi wa Dar es Salaam,
 Robert Massawe (51) ambaye 
polisi wanadai ni mtuhumiwa 
hatari wa uporaji na mauaji
 ameuawa kwa kupigwa risasi
 na watu wanaodaiwa kuwa ni 
wenzake.

Kabla ya kuuawa katika majibizano 
ya risasi, mtuhumiwa huyo anadaiwa 
kukamatwa na bunduki aina ya SMG
 ikiwa na risasi 24, simu 19 
zilizoporwa maeneo mbalimbali 
na laini za simu 58. Taarifa 
iliyotolewa jana na kamanda 
wa polisi mkoani Kilimanjaro,
 Hamisi Issah ilisema mtuhumiwa
 huyo aliuawa juzi saa tisa alfajiri 
wilayani Rombo na watu 
wanaodaiwa kuwa watuhumiwa
 wenzake.Kwa mujibu wa taarifa
 hiyo, mtuhumiwa huyo pamoja 
na mkewe walikamatwa 
jijini Dar es Salaam na baada 
ya kuhojiwa na polisi anadaiwa
 kueleza matukio mbalimbali 
ya ujambazi aliyoshiriki.
Kamanda Issah alisema baada
 ya kukamatwa jijini humo na
 kuwaeleza polisi ushiriki wake
 katika matukio mbalimbali ya
 ujambazi alikubali kuwaonyesha
 mahala alipoficha bunduki hiyo.

Polisi waliandamana naye
 chini ya ulinzi mkali hadi 
Moshi kwenye dampo lililopo
 karibu na kiwanda cha ngozi 
ambapo bunduki ilipatikana
 ikiwa imefukiwa ardhini 
ikiwa na risasi 24. “Muda 
wote alitoa ushirikiano
 mkubwa kwa polisi na
 alivyokuwa akisimulia 
matukio aliyoyafanya mwili 
unaweza kusisimka. 
Simu tatu kati ya 19 
tumegundua ziliporwa
 hapa Moshi,” alisema.

Katika mahojiano hayo 
inadaiwa mtuhumiwa 
huyo aliwaeleza polisi juu ya 
mpango uliokuwapo wa 
kufanya tukio la ujambaz
katika kijiji cha Chilio, kata 
ya Holili wilayani Rombo juzi
 alifajiri.“Akiwa chini ya 
ulinzi wa askari kanzu
 alikubali kuwapeleka
 polisi katika eneo hilo, 
sasa walipofika alipowaona 
wenzake alipiga kelele ya 
kuwajulisha wenzake kuwa 
polisi walikuwapo eneo hilo,” 
alisema.