Zlatan Ibrahimovic na Paul
Pogba wataorodheshwa katika
kikosi cha Manchester United
katika mechi ya Jumamosi ya
ligi ya Uingereza dhidi ya
Newcastle katika uwanja wa
Old Trafford.
Mshambuliaji Ibrahimovic , 36,
bado hajashirikishwa katika
mechi yoyote msimu huu baada
ya kupata jeraha la goti mnamo
mwezi Aprili.
Kiungo wa kati Paul Pogba ,
24, hajaichezea timu yake tangu
alipopata jeraha la nyuma ya goti
dhidi ya klabu ya Basel mnamo
mwezi Septemba.
Beki Marcos Rojo pia anapatikana
na mkufunzi Jose Mourinho
alisema kuwa wote wataorodheshwa.
''Paul unaweza kuona. Unaweza
kugundua kwamba kulikuwa
na Manchester United msimu
huu kabla na hata baada ya
jeraha lake'', aliongezea Mourinho.
''Ana uwezo ambao hubadilisha
vile tutakavyocheza mechi zetu''.
Mshambuliaji wa zamani wa
Sweden Ibrahimovic ameichezea
klabu hiyo mechi 46 na kufunga
magoli 28 msimu uliopita.
Aliachiliwa na klabu hiyo mnamo
mwezi Juni baada ya msimu
wake kumalizwa na jereha la
nyuma ya goti lakini akapewa
mkataba mwengine mpya wa
mwaka mmoja mnamo mwezi Agosti.
''Msimu uliopita tulimchezesha
Zlatan kila dakika'', aliongezea
Mourinho.
''Tulijifunza kucheza bila yeye.Lakini
tunamkaribisha ni mchezaji mzuri sana''.

0 Comments