Na Thomas Ng’itu
Timu ya Ndanda imechapwa bao moja kwa sifuri na Yanga, mechi inayowafanya Yanga kusogea mpaka nafasi ya tatu wakiwa na pointi nane.

Katika mchezo huo Ndanda walionekana kujilinda zaidi kuliko kushambulia, kutokana na jinsi aina ya uchezaji wao ukivyokuwa.
Ndanda kwenye kipindi cha kwanza walimsimamisha Omary Mponda mbele akiwa peke yake, huku akikabwa na beki Kelvin Yondani mwenye uzoefu wa kutosha akisaidiana na Andrew Vincent.
Katika nafasi ya katikati Yanga waliwaweza Ndanda kwa kuwachezesha Papy Tshishimbi, Thabaan Kamusoko na Raphael Daud kwasababu viungo wote hawa wanauwezo wa kupokonya mipira na kusambaza kwa haraka.
Ndanda walikuwa wakijikaba baada ya Jabir Aziz ‘Stima’ na Rajab Zahir kuwa wanacheza chini zaidi, hali iliyowafanya viungo wa Yanga kutawala dimba la kati.
Katika beki ya kati iliyokuwa ikiongozwa na Hamad Wazir ‘Kuku’ na Hemed Khoja walikuwa hawana utulivu kwani ilikuwa ni butua butua ya kuondoa mashambulizi, lakini mipira mbele ilikuwa haikai kutokana na kutokuwa na mtu wa kusaidiana na Mponda.
Mabeki wa pembeni William Lucian na ayoub Masoud walikuwa na kazi kubwa ya kukaba na hata walipokuwa wakipeleka mashambulizi mipira ilikuwa haikai mbele.
Kipindi cha pili Kocha Malale Hamsini alimuingiza Kelvin Friday na kwenda kusaidiana na Omar Mponda katika nafasi ya ushambuliaji, bado walionekana kutokuwa na maelewano mazuri ya kupitiliza.
WAFANYE NINI
Ndanda kwa matokeo yao bado wana uwezo wa kufanya vizuri kikubwa wampe muda kocha wao Hamsin Malale kutokana na timu hiyo kuwa na mchanganyiko wa wachezaji wengi wapya ambao wanatakiwa wapate kujuana kwenye takribani mechi tano.
Uvumilivu ndio utakaowafanya wafanye vizuri katika ligi na sio jambo lingine lolote la nje ya uwanja wanalolifikilia.
MATOKEO
Ndanda 0-1 Azam
Mbeya City 0-1 Ndanda
Prison 0-0 Ndanda
Yanga 1- 0Ndanda