
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu wawili kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 44 walizokuwa wakisafirisha kutoka Sirali kwenda mwanza kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Watu hao wawili waliofahamika kwa majina ya James Lawrence mwenye umri wa miaka 51, mkazi wa Tarime mkoani Mara, amekamatwa akiwa na mirungi kiasi cha kilo 35, aliyokuwa akisafirisha toka Sirali kwenda Mwanza kwenye bus lenye namba T.498 DAK, aina ya Youtong, na Magabe Mirumbe mwenye umri wa miaka 45, mkazi wa Tarime mkoani Mara, amekutwa na mirungi kiasi cha kilo 09, aliyokuwa akisafirisha kutoka Sirali kwenda Mwanza kwenye bus lenye namba T. 201 DAN aina ya Youtong, jana Septemba 22 majira ya saa mbili usiku.
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mwanza inasema kuwa askari walikuwa kwenye kizuizi tajwa hapo juu wakisimamisha na kupekua magari yote yaliyokuwa yakipita kwenye barabara ya mwanza kwenda musoma, ili kuweza kubaini madereva na abiria wanaosafirisha madawa ya kulevya. aidha wakati wakiendelea kusimamisha na kupekua magari hayo waliweza kukamata magari tajwa hapo juu yakiwa na abiria hao waliokuwa wakisafirisha mirungi.
0 Comments