Aslay Afunguka Bifu Lake na Beka Asema Wao ni Washkaji Mashabiki ndo Wanakuza


HUKU kukiwa na fununu
 za kuwepo kwa bifu zito
 kati ya Aslay
 namwanamuziki 
mwenzake Beka Flavor,
 ambao walifanya kazi 
pamoja katika Yamoto
Band, msanii huyo
amefunguka kuwa 
hakuna bifu lolote kati
 yao.Akizungumza na Risasi
Vibes, Aslay alisema kwa muda 
mrefuamekuwa akihusishwa
 kuwa katika msigano na Beka 
Flavor kitu mbacho si kweli 
kwani waoni washkaji licha 
ya kutofanyakazi pamoja kwa
 sasa.“Mimi na Beka ni washkaji 
vibaya sana, tena mara ya mwisho 
kuwasiliana naye ilikuwa jana (juzi), 
mashabiki ndiyo wanakuza 
mambo hayo lakini ukweli ni
kwamnba sina bifu na Beka,”
 alisema Aslay.