Simbeye Anusurika Kifo Baada ya Kupata Ajali ya Gari


Katibu Mwenezi wa Baraza la 
Vijana wa Chama 
cha Demokrasia na Maendeleo
 (Bavicha), Edward 
Simbeye amepata ajali ya
 gari.
Simbeye alikuwa akitokea
Dar es Salaam kwenda Moshi 
mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Mwananchi
 leo Jumatano asubuhi, 
Simbeye amesema ajali hiyo
 ilisababishwa na tairi la 
mbele kushoto kufyatuka
 hivyo gari kupoteza 
mwelekeo na kuanguka
kando mwa barabara eneo
 la Kawawa mjini Moshi.

“Namshukuru Mungu
nimetoka salama
 mimi na mdogo wangu…
nilikuwa 
nakwenda nyumbani
kwa sababu za 
kifamilia,” amesema
 Simbeye.