Rais Magufuli Kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM




Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi 
(CCM) inakutana jijini Dar es Salaam 
chini ya Mwenyekiti Rais John Magufuli.

Kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika
 leo Jumatatu Novemba 20,2017
 kitafuatiwa na kingine cha
 Halmashauri Kuu ya Taifa kesho 
Jumanne Novemba 21,2017.

Taarifa iliyotolewa awali na Katibu
 wa Itikadi na Uenezi ya CCM,
 Humphrey Polepole imesema vikao
 hivyo pamoja na mambo mengine 
vitakuwa na ajenda ya kupokea 
tathmini ya uchaguzi mdogo wa 
udiwani katika kata 43 ambao kampeni
 zake zinaendelea.

“Ajenda nyingine ya vikao hivi vya 
uongozi vya kitaifa itakuwa kupokea, 
kuchuja, kutoa mapendekezo na
 kufanya uteuzi wa mwisho katika 
ngazi ya mikoa na taifa katika chama 
na jumuiya zake kwa maana ya umoja
 wa vijana, wanawake na wazazi,”
 ilisema taarifa ya Polepole.

CCM sasa ipo katika mchakato wa uchaguzi 
wa ndani kuanzia ngazi ya shina mpaka taifa

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi 
(CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana 
akithibitisha kutimia kwa akidi kabla 
ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu 
ya CCM jijini Dar es salaam
 kinachoongozwa na Mwenyekiti wa 
chama hicho Rais Dkt. John Pombe 
Magufuli leo Jumatatu Novemba 20, 2017