Dkt Shika Apata Shavu la Matangazo na Huu ndo Muonekano Wake Mpya



Maisha ya Dk Louis Shika ambaye
 hivi karibuni aliingia kwenye 
headline baada ya kushindwa 
kutoa asilimia 25 ya mnada wa 
nyumba za Lugumi muda mchache
 baada ya kushinda mnada huo, 
yameanza kubadilika taratibu
 kutokana na kupata deal kadhaa
 za matangazo.

DK Shika ambaye alikuwa katika
 muonekano ambao haufananii na 
utajiri anaoutangaza kuwa nao, 
weekend hii ameonekana akiwa 
amevaa suti kali.


Wadau wa mambo wanadai kuwa 
mzee huyo mashuhuri mitandaoni
 amepata deal kubwa katika 
kampuni moja kubwa la michezo
ya kubashiri.

Huwenda akapata deal nyingi zaidi
 kutoka na umaarufu alionao kwa sasa