Uwanja Mkuu wa Ndege Zimbabwe Wapewa Jina la Rais Robert Mugabe


Uwanja mkuu wa ndege nchini 
Zimbabwe umebadilishwa jina na 
kupewa rasmi jina la Rais Robert 
Mugabe.
Uwanja wa Kimataifa wa Harare 
sasa utaitwa uwanja wa Kimataifa
 wa Robert Mugabe.
Mtandao mmoja wa habari ulichapisha 
picha za sherehe hizo zilizofanyika mji 
mkuu Harare.

Barua kutoka kwa mamlaka za safari 
za ndege nchini humo kushauri kuhusu 
mabadiliko hayo ilisambatwa pakubwa
 kwenye mtandao wa Twitter mwezi 
SeptembaMugabe, 93, ameitawala nchi 
hiyo tangu mwaka 1980.