Mmoja wa Madiwani ambao
wamehamia 
CCM wakitoka CHADEMA 
mkoani Arusha waliokumbwa
 na skendo 
ya kununuliwa, amemtaka 
Mwenyekiti 
wa chama hicho Freeman 
Mbowe,
 kumtafuta aliyekuwa
 katibu wake
 Mkuu Wilbroad Slaa, 
ili kuokoa jahazi 
kwenye chama.Kwenye 
video ambayo
 anaonekana akizungumza,  
aliyekuwa 
diwani wa kata ya
 Kimandolu Mchungaji 
Rayson Ngowi, amesema 
kuna haja ya kutafuta
 hekima za Wilbroad Slaa, 
ili kukisaidia chama 
hicho kukaa kwenye mstari 
unaofaa, kwa kuwa 
sasa kimeanguka kwa 
kiasi kikubwa.
Bwana Ngowi amesema
hata yeye kutoka 
CHADEMA ameondoka
kwa kutaka mwenyewe 
na sio kununuliwa kama
 inavyodaiwa, na 
kwamba kuna wengine
watakaofuata nyuma
 yao baada ya wao
kuondoka kwenye chama
hicho.
“CHADEMA ya leo sio
 ile ya Dkt Slaa, CHADEMA
yaleo ni  ya maslahi,
 CHADEMA ganganjaa, na
wakikataa mimi nitasema,
sikiliza Mbowe, chama 
chako kina matatizo
makubwa, huna viongozi,
 kamtafute Dkt. Slaa
nafikiri ataokoa jahazi,
 kama mnataka kurudisha
 imani, kwa sababu sio
 mimi tu nimeondoka
watakuja wengi”,
amesema
 diwani huyo.