Zitto Kukimbilia Mahakamani Kupinga Uteuzi wa Rais Magufuli



Mbunge wa Kigoma Mjini,
Zitto
 Kabwe (ACT-Wazalendo)
 amesema
 Jumatano hii ataenda
 Mahakamani
 kupinga uteuzi wa nafasi
ya Katibu 
wa Bunge uliofanywa na
Rais wa
 Jamhuri ya Muungano wa
 Tanzania 
Dkt.John Pombe Magufuli
Jumamosi 
iliyopita.Uteuzi huo ulienda
 sambamba 
na uteuzi wa Mawaziri 
ambapo baadhi ya 
mawaziri walibadilishwa 
na wengine 
kuongezwa.“Katika
kulinda utawala wa 
sheria nchini kwetu, 
pia Uhuru na Hadhi ya
 Mhimili wa Bunge, Leo 
tarehe 11/10/2017 
tunawasilisha mahakamani 
ombi la kutengua
 uteuzi wa Katibu wa 
Bunge na kutaka 
mchakato wa kisheria 
ufuatwe katika kumpata
 Katibu wa Bunge la
 Jamhuri ya Muungano
 wa Tanzania,” aliandika 
Zitto Facebook.
Rais Magufuli alimteua 
Katibu mpya wa 
Bunge na yule ambaye
 alikuwa akifanya
shughuli hiyo 
kuahidi kumpangiwa kazi
nyingine.
Zitto alisema uteuzi wa
Katibu wa Bunge 
uliofanywa na Rais John
Magufuli ni batili Kwa 
mujibu wa Sheria ya
 Utawala wa Bunge, sheria
 namba 14 ya mwaka 2008
 ikisomwa pamoja na
 Katiba ya JMT ibara ya
 87.Alisema Katiba inatoa 
Mamlaka Kwa Rais kuteua na 
sheria inaweka utaratibu Wa
 kutekeleza mamlaka hayo ya
 Katiba.