Image result for Irene UwoyaImage result for Irene UwoyaImage result for Irene UwoyaImage result for Irene Uwoya

FAMILIA ya aliyekuwa Kocha 
Msaidizi wa Timu ya Rayon Sports
 ya Rwanda, Hamad Ndikumana
 ‘Katauti’ (39), imezuia staa wa 
filamu Bongo, Irene Uwoya ambaye
 alikuwa mke wa jamaa huyo asifanyiwe 
fujo baada ya kutinga nchini 
Rwanda jioni ya Ijumaa iliyopita.
 Hatua hiyo ilikuja baada ya 
Ndikumana kupoteza maisha huku 
Uwoya akishushiwa tuhuma za hapa 
na pale na kwamba huenda alichangia
 kifo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo chetu 
kilichoambatana na Uwoya, familia 
ya Ndikumana ilichukua uamuzi huo 
baada ya watu mbalimbali nchini humo 
kuwa na hasira na Uwoya. Kutokana 
na kifo cha Ndikumana, Uwoya 
alilazimika kwenda Rwanda kuhani 
msiba akiwa na mwanaye aliyezaa na 
jamaa huyo, Krish, mama na baba
 yake na mabaunsa wa kumpa ulinzi.

Chanzo hicho kilieleza kwamba, watu 
mbalimbali nchini humo walikuwa na
 hasira juu ya Uwoya kwamba ndiye 
aliyesababisha kifo cha Ndikumana
 kwani alikuwa na msongo wa mawazo
 akimfikiria yeye kwa kuwa alimpenda 
na kutaka wairudishe ndoa yao, 
lakini mwanamama huyo akawa
 anang’ang’ania apewe talaka
 ambayo hadi Ndikumana anafariki 
dunia alikuwa hajaitoa.

Staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya.
“Mashabiki wa Ndikumana walitaka 
kumfanyia fujo Uwoya kwa kuwa 
wanadai ndiye chanzo cha kifo cha
 mpendwa wao, lakini familia
 iliwazuia wasifanye hivyo kwa
 kuwa walishamsamehe Uwoya 
ndipo hali ya amani ikawepo,”
 kilisema chanzo hicho. Kiliendelea
 kueleza kuwa, Uwoya aliwasili 
nchini Rwanda Ijumaa iliyopita
 kwenda kuona kaburi la mumewe
 ambaye alizikwa Jumatano iliyopita
 ambapo alipokelewa vizuri na 
mama wa Ndikumana pamoja na
 familia kwa jumla.

“Zile tofauti waliziweka pembeni 
na mama Ndikumana akamwambia
 wamemsamehe hivyo ikawa ni
 kuomboleza upya kwani Uwoya
 na mama’ke alikuwa akilia sana 
hadi kushindwa kutembea
,” kilisema chanzo hicho. Hata 
hivyo, alisaidiwa kwa kushikwa 
mkono na wenyeji kwani mama 
huyo alikuwa akimpenda sana 
mkwewe Ndikumana kama mtoto wake.

Baada ya chanzo kutiririka, Ijumaa 
Wikienda lilimtafuta Uwoya ambaye
 alikiri kupokelewa vizuri na familia 
pamoja na mama Ndiku ambaye
 alipomuona tu alimkumbatia huku 
akilia kwa uchungu akimuita ‘mwanangu’.
 Naye msanii wa filamu, Michael
 Sangu ‘Mike’ ambaye ni mmoja
 wa watu waliosafiri alikiri kuwa 
walipokelewa vizuri na hakuna
 tofauti yoyote iliyojitokeza.

“Uwoya, baba, mama na Krish
 walitangulia na ndege na 
walipokelewa vizuri kabisa na 
hakuna mtu aliyewafanyia fujo
 wala nini, familia imewapokea
 kwa ukarimu na sisi ambao 
tulifika baadaye maana tulisafiri
 kwa basi tulipokelewa vizuri 
sana,” alisema Mike Sangu.
Chanzo: Global Publishers